Sunday, March 19, 2017

KILIMO CHA MBAAZI NA KANGETAKILIMO







KILIMO BORA CHA MBAAZI NA KANGETA KILIMO
             








Utangulizi

 Mbaazi nizao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara Mbaazi inakiasi kikubwa cha protini.Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 4 kwa hekari moja
 Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulima zao hili. ni zao  ambalo linalo stahamili ukame na pia hupendeza sana kama likipandwa pamoja na mazao mengine kama mihogo au mahindi  zao hili Huhitaji mazingira ya joto, kuanzia nyuzi joto 25-40 sentigrade


 
UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
 unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi (Clay soil) –
 unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
• Tindikali ya udongo
• Kiasi cha mboji
• Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.

Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).


AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LA MBAAZI
 Mbaazi zina stawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.

AINA KUU ZA MIMEA YA  MBAAZI
  Kuna aina tatu za mimea ya mbaazi
1)
Mbaazi za muda mrefu:         
Hii ni mbaazi ambazo zinaweza kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake nakuruhusu Machipukizi yake kukua na kuvunwa tena msimu unao fuata na zoezi hili hufanyika zaidi ya msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa

 

2>Mbaazi za Muda wakati;
Hizi hulimwa kwa msimu mmoja ila huchukua mda wa katika kukomaa kwake.huchukua muda wa siku 140 hadi 180








3)MbaazizamudaMfupi:
Hizi hulimwa kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung'olewa nakupandwa mbegu mpya msimu unaofuata.mbegu huchukua muda wa siku 120 hadi 140.



UANDAJI WA SHAMBA SHAMBA
Andaa shamba kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya
kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda mbegu zako za mbaazi.
Hakikasha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini. Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa mbaazi huhitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha

UPANDAJI

1>Mbaazi za Muda Mrefu;
Panda kwa mistari kwaumbali wa sentimeta 150 kwa 100.
     (Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika mstari)

2>Mbaaziza Muda wa Kati;
Mbaazi. Panda kwa mstari na kiasi cha sentimeta 100  kwa 60

3>Mbaaziza Muda  Mifupi;
Panda kwamstari  kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwasentimeta 60


MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile: 
i.                    Mbolea vunde:
 inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii.                  Samadi:
 kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
iii.                Mbolea za kijani:
hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na     kuchanganywa na udongo.
iv.                Majivu:
ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v.                  Matandazo (mulch):
ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.


Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

Mbolea Za Kupandia
Mbolea maarufu za kupandia katika soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao. Lakini zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa ‘Kukuza matumizi ya Minjingu Phosphate’ ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.

                  1. Diammonium Phosphate (DAP)
Ina virutubisho viwili - naitrojeni ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 18, na fosfati (P2O5) ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 46. Inapatikana katika hali ya chengachenga (granules).


             2. Minjingu Phosphate
Ina kiwango cha fosfati (P2O5) asilimia 29 na inatumika zaidi kwa kutoa kirutubisho hiki. Lakini inaongeza vilevile kirutubisho cha chokaa (calcium) ambacho kipo kwa kiwango cha asilimia 40. Chokaa inasaidia vilevile kukabili tindikali (acidity) ya udongo.

                    
            3. Minjingu Mazao
Hii ni mbolea mpya inayotokana na Minjingu Phosphate lakini imeongezwa virutubisho vingine vitano ambavyo ni naitrojeni (10%), salfa (5%), zinki (0.5%), shaba (0.5%), boroni (0.1%), pamoja na chokaa (25% CaO) na magnesium (1.5% MgO). Virutubisho vilivyoongezwa hususani naitrojeni na salfa ni vile ambavyo vinakosekana katika aina nyingi za udongo.
Zinki, shaba na boroni vimeongezwa kwa tahadhari kwa sababu vinaonyesha dalili za upungufu katika baadhi ya maeneo. Minjingu Mazao iko katika hali ya chengachenga.

namna ya kuchagua mbolea ya kupandia
Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya 6.2 ili mbolea za Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye tindikali zaidi ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa potashi, tumia mbolea zinazorejesha madini hayo.

Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza mazao. Mboji huwa haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha mbolea na mbegu).

1. Upungufu Wa Naitrojeni (Nitrogen)
Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo, na mwishowe hutoa mazao kidogo . Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza usitoe mazao. Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha mmea kudumaa. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa sana, majani hugeuka rangi ya njano kutoka pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza kugeuka.Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha.


2. Upungufu Wa Fosfati (Phosphorus)
Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba. Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye mashina na baadaye husambaa kwenye jani lote. Rangi inaonekana vizuri zaidi upande wa chini wa jani. Majani ya mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.
 

3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)
Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea kudumaa.
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi , mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye ncha. Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.


JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI  WA  KUPANDA
Wakati wa kupanda, mbolea kama vile Yara Miller Winner, au NPK, DAP, MiNJINGU AU TSP, zitakufaa, ila ni bora zaidi kama utatumia DAP kipimo kama gram10 sawa na kifuniko kimoja cha maji ya uhai mfuko 1 unatosha kwa hekari moja angalizo mbolea a viwandani zisichanganyike na mbegu. kama utatumia samadi ni vizuri zaidi kiasi cha mkokoteni 1 kitatosha kwa hekari moja ila kama utatumia samadi hakikisha ukisha iweka kwenye masimo acha kwa muda wa wiki moja alafu panda

JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI  WA KUKUZIA MBAAZI
Utahitaji mbolea kama vile, CAN, UREA, AU NPK, Au Yara Miller winner, changua moja kati ya hizo kipimo ni Gram  10 sawa na kifuniko cha soda au maji safi kwa kila mmea kwa hekari moja utatumia kama  mfuko mmoja

MAVUNO
Mavuno kwa ekari moja ni kati ya tani 1 hadi 4, yaani( gunia 10 hadi 40 za uzito wa kilo 100)



WADUDU WANAOSHAMBULIA MIBAAZI  NA MBAAZI
WADUDU WA HARIBIFU
1.      Funza wa matunda
2. Funza wa katika mimea ikiwa michanga
3.Mnyauko (Fusarium Wilt)
5. Ukungu-Fangasi
 Mbaazi ni moja wapo ya mazao ambayo hayashambuliwi sana na wadudu japo kuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi. Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama  vile Attakan-c,Karate au dawa nyingine za wadudu.
2.    MAGONJWA YA MBAAZI  
Madawa ya kutumia kuzuia ukungu ni kama vile
1. Ridomil Gold 2. Ebony (Mancozeb +Metalaxyn), 3, Ivory, 4.Nordoxetc
magonjwa makuu yanaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa fusaria ( fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi nyeusi,ugoro au kahawia.ugonjwa huu huzuia mfumo mkubwa wa ukuaji wa mmea.Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani kila baada ya msimu kuisha.usipande kila msimu mbaazi tuu.Kilamsimu badilisha mazao.

UVUNAJI WA MBAAZI

Mbaazi zikisha komaa nakuanza kukauka zivunwe mapema kwakukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kasha .Mbaazi zitenganishwe kwa mikono au kwakupigwa hayo matawi  taratibu  baada ya kukaushwa sana.
   

HIZI NDIZO AINA BORA ZA MBEGU ZA MBAAZI



MUDA WA KUOTA MBEGU
Tangu kupanda mbegu hadi kuota huchua siku 4 hadi 21, na baada ya hapo mimimea huanza kukua polepole, hivyo hakikisha unazuia magugu

MUDA WA KUKOMAA
Tangu kupanda hadi kutoa maua,huchukua siku 60 hadi 80, na baadaya maua huchukua siku 50-75 kutengeneza mbegu zilizokomaa, hivyo huchukua kati ya miezi 5 hadi 6 kukomaaa
IDADI YA MBEGU KWA EKARI 1
KILO 10 hutosha kwa ekari moja, kama unaweka mbegu mbili mbili kwa kila shimo, na kilo 5 hutosha kwa ekari moja kama unaweka mojamoja kwa kila shimo


  Mwisho wa makala
 (kangetakilimo) +255717274387:web :kangetakilimo email: emmanuelkangeta@gmail.com  
  fb:kangetakilimo   whatssap:+255717274387


                                       Free master plan and cost benefits analysis(CBA)




No comments:

Post a Comment