Thursday, March 1, 2018

KILIMO BORA CHA MAHINDI NA KANGETA KILIMO


                                                                                                            Agro Project Tz 










                                                     
                                                
 EMMANUEL KANGETA
tell:+255717274387
Whats app: +255717274387
email:emmanuelkangeta@gmail.com
Email:kangetakilimo@gmail.com
web:kangetakilimo
Fb :kangetakilimo 
Fbgroup:dondoo za kilimo
………………...
KILIMO CHA MAHINDI

Mahindi huwezwa kulimwa na kustawi vizuri katika uwanda wa chini kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2500 kutoka usawa wa bahari.Mahindi mengine hukubali vizuri katika ukanda wa chini na mengine katika ukanda wa juu.hukua vizuri katika maeneo yapatayo mvua za kutosha kiasi cha milimita 750 na kuendelea kwa mwaka hustawi katika nyuzi joto 22 -33 C.Pia ktokana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni  

MCHANGANUO KWA HEKA MOJA
kwa space ya upandaji 75cm(mstari na mstari)-25cm(mche na mche) utakuwa na  miche 5300 kwa space ya 90-30 utakuwa na miche 3700 tuannze na space ya 75cm-25cm utakuwa na miche 5300 kwa mbegu za chotara hubeba mahindi mawili hadi matatu chukua kila mche mmoja unamahindi mawili utakuwa na jumla ya mahindi(5300miche zidisha mara 2 idadi ya mahindi ktk mche mmoja=10600 jumla ya mahindi kwa heka moja)kwa kipindi cha mwezi wa tisa hadi masika indi moja bichi huwa linauzwa 500tsh je?heka moja utakuwa na shilingi ngapi chukua sasa jumla ya mahindi zidisha mara mia tano(10600 zidisha 500=5300000tsh) kwa heka moja ya mahindi utapata shillingi milioni tano na laki tatu

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MAHINDI
Mahitaji ya udongo na mbolea ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mmea wowote ule, hata hivo mahitaji hayo hutofautiana kati ya mmea moja na mwingine kutokana na kutofautiana kwa sehemu ya zao  katika hiyo mimea (yaani economic part of a plant). Kwa mfano: mahindi
Udongo una rutuba ya asili yaani virutubisho katika udongo, mboji (organic matter), na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye udongo. Rutuba ya udongo inategemea sana hali ya udongo kikemia, kibiolojia na kifizikia.

 AINA ZA UDONGO
Kuna aina   tatu ya udongo ambazo ni
Ø  Kichanga (Sand soil)
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
Ø  Tifutifu (Loam soil)
 unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
Ø  Mfinyanzi (Clay soil)
 unahifahdi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mdogo.

Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
ü  Tindikali ya udongo
ü  Kiasi cha mboji
ü  Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.

 SOIL PH
pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).
Mahindi hustawi kwenye udongo wa tifutifu wenye tindikali ya wastani na virutubisho vya kutosha.

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MAHINDI
Hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH ya 6 hadi 7.hukubali katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.unaweza kulima katika udongo wa kichanga au mfinyanzi japokuwa katika udongo wa mfinyazi kama mvua itakuwa kubwa na maji yakatuama kwa muda mrefu huzuia ukuaji mzuri wa Mahindi.

MAANDALIZI YA SHAMBA
Taarisha shamba lako la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Magonjwa kama yale ya majani(streak ugonjwa wa milia) hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi na yatastawi vizuri. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kungoa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
  1. Jembe la mkono - wengi wanatumia
  2. Jembe la kukokotwa na wanyama kama ngombe
  3. Power tillers
  4. trekta
MUDA WA KUPANDA KATIKA MAENEO YA TANZANIA
Wakati wa kupanda  kwani mvua haitabiriki,Kama mvua hunyesha nyakati na
majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la
mahindi katika maeneo ya TANZANIA . mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni., Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati. mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni , Novemba hadi Januari mwanzoni.Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvuakuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama wengineo.

AINA ZA MBEGU

AINA ZA MBEGU
 Kuna aina kama tatu za mbegu za mahindi
v  1) Mbegu aina ya chotara (hybrid)
 2) Aina ya ndugu moja(synthetic)
  3) Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5
7.5 kwa hekta moja. Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa
Ø   SIDCO ,
Ø  MH501
Ø  PANNAR,
Ø  CHOTARA,
Ø  TMV1, TAN 250,
Ø  TAN 254, Staha, Situka,na zingine zote zinazoanza na herufi H kama vile H 250, H 251 na H 615. Pia mbegu mpya zilizotangazwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka huu ni WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115


MBEGU BORA ZA MAHINDI NA SIFA ZAKE

Kituo cha utafiti ilonga
Ø  Mahindi WE4106
Aina hii ni mahindi chotara.
Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
Bahari.
·Inakomaa Kwa wastani wa siku 106.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa   mahindi (grey leaf spot) na kutu yamajani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

Ø Mahindi WE4102
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
bahari.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 105.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu
wa mahindi (grey leaf spot) na kutu yamajani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.7kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

Ø Mahindi WE4110
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
bahari.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 101 hadi 111.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa       majani (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability)
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.6 kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

Ø Mahindi WE4114
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na katiwa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
  bahari.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 102.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia yamahindi (maize streak), bakajani kijivu wa    mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.9 kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

Ø Mahindi WE4115
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
   bahari.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 112.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), bakajani kijivu wa   mahindi (grey leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.4,kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

Ø Mahindi WE4112
 ·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na kati wa mita 0 hadi 1,500 kutoka usawa wa
   bahari.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 103.
·Ina ukinzani wa magonjwa ya milia ya mahindi (maize streak), Ukungu kijivu
  wa mahindi (grey Leaf spot) na kutu ya majani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability)
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.5 kwa hekta.
·Inastahimili ukame.

2. Kituo cha Utafiti Selian
Ø Mahindi  Selian H215
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa kati ya siku 105 hadi 148.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5 kwa hekta.
·Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) hususan
katika maeneo ya kanda ya kaskazini

3. Kituo cha Utafiti Tumbi
Ø Mahindi T104
·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
·Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,500.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 104 hadi 128.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.5 kwa hekta.

Ø Mahindi T105
·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV)
·Inastawi katika ukanda wa kati katika mwinuko wa mita 600 hadi 1500.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 103 hadi 129.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.4 kwa hekta.

4. Aminata Quality Seeds & Consultancy Ltd

Ø Mahindi NATA H401
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 400 hadi 1,500.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 120 hadi 130.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7 kwa hekta.
·Inastahimili ugonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot), baka jani   (leaf blight) na kutu ya majani (leaf rust).
·Inakoboleka vizuri (good poundability).

Ø Mahindi NATA K 8
·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
·Inastawi katika ukanda wa chini na kati katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,600.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 110 hadi 120.
·Inastahimili magonjwa ya bakajani wa mahindi (grey leaf spot), milia ( maize
streak virus) na ‘Turcicum blight’.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.9 kwa hekta.

5. Krishna Seed Company Ltd
Ø Mahindi Krishna Hybrid-1
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa kwa muda wa siku 128.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.9 kwa hekta.
·Inastahimili magonjwa ya majani wa ukungu kijivu wa mahindi (grey leafspot)  milia ya mahindi (maize streak virus).

Ø Mahindi Krishna Hybrid-2
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Inastawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa kwa muda wa siku 134.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 7.6 kwa hekta.
·Inastahimili magonjwa ya ukungu kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).

6. Meru Agro-Tours & Consultancy Co. Ltd
Ø Mahindi MERU LISHE 503
·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
·Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
·Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa mapema kwa wastani wa siku99.
·Ina stahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi(grey leaf spot)na milia ya mahindi ( maize streak virus).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 4.3kwa hekta.
·Inakoboleka kirahisi.

Ø Mahindi LISHE 511
·Aina hii ni mahindi ya kawaida (OPV).
·Aina ya mahindi lishe yaliyo na kiwango kikubwa cha viini muhimu vya protini.
·Hustawi katika mwinuko wa mita 800-1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa kwa muda wa wastani wa siku 98.
· Ina ukinzani wa magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na
milia ya mahindi ( maize streak virus).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 5.2 kwa hekta.
·Inakoboleka kirahisi.

6. IFFA Seed Company Ltd
Ø Mahindi Kaspidi hybrid
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Hustawi katika mwinuko wa mita 600 hadi 1,200 kutoka usawa wa bahari.
·Inakomaa kwa muda wa siku 150 hadi siku 155.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.1 kwa hekta.
·Inastahimili magonjwa wa bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya mahindi (maize streak virus).

Ø Mahindi Kisongo hybrid
·Aina hii ni mahindi chotara.
·Hustawi katika ukanda wa mwinuko wa mita 600 had 1,200 kutoka usawa wa
bahari.
·Inakomaa katika siku 138.
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 6.8 kwa hekta.
·Inastahimili magonjwa ya bakajani kijivu wa mahindi (grey leaf spot) na milia ya   mahindi (maize streak virus).

Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya
v  Mwinuko kutoka usawa wa bahari
v  Kiasi cha mvua katika eneo husika
v  Muda unaotumia mbegu
v  hadi kukomaa
NAMNA YA KUPADA
Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu)Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., Hii hutegemea na aina ya mbegu Hiyo ni baina ya mstari na mstari na mche kwa mche. 75cm mstari kwa mastari x 25cm mche na mche nafasi hii utakuwa na miche 5300 kwa hekari mja kwa maeneo yenye mvua nyingi 90cm x 30cm utakuwa na miche 3700 kwa hekar mja kwa maeneo yenye mvua chache

MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
    2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile: 
     i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
      ii.  Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
     iii.  Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
    iv.  Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
      v.  Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

Mbolea Za Kupandia Mahindi
Mbolea maarufu za kupandia katika soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao. Lakini zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa Kukuza matumizi ya Minjingu Phosphate ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.

                  1.Diammonium Phosphate (DAP)
Ina virutubisho viwili - naitrojeni ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 18, na fosfati (P2O5) ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 46. Inapatikana katika hali ya chengachenga (granules).




                     2. Minjingu Phosphate
Ina kiwango cha fosfati (P2O5) asilimia 29 na inatumika zaidi kwa kutoa kirutubisho hiki. Lakini inaongeza vilevile kirutubisho cha chokaa (calcium) ambacho kipo kwa kiwango cha asilimia 40. Chokaa inasaidia vilevile kukabili tindikali (acidity) ya udongo.



                     3. Minjingu Mazao
Hii ni mbolea mpya inayotokana na Minjingu Phosphate lakini imeongezwa virutubisho vingine vitano ambavyo ni naitrojeni (10%), salfa (5%), zinki (0.5%), shaba (0.5%), boroni (0.1%), pamoja na chokaa (25% CaO) na magnesium (1.5% MgO). Virutubisho vilivyoongezwa hususani naitrojeni na salfa ni vile ambavyo vinakosekana katika aina nyingi za udongo.
Zinki, shaba na boroni vimeongezwa kwa tahadhari kwa sababu vinaonyesha dalili za upungufu katika baadhi ya maeneo. Minjingu Mazao iko katika hali ya chengachenga.

Jinsi ya kuchagua mbolea ya kupandia
Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya 6.2 ili mbolea za Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye tindikali zaidi ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa potashi, tumia mbolea zinazorejesha madini hayo.

Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza mazao. Mboji huwa haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha mbolea na mbegu).

Dalili Ya Upungufu Wa Virutubisho Mbalimbali
1. Upungufu Wa Naitrojeni (Nitrogen)
Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo, na mwishowe hutoa mazao kidogo  Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza usitoe mhindi kabisa.

Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha mmea kudumaa. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa sana, majani hugeuka rangi ya njano kutoka pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza kugeuka. Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha.




2. Upungufu Wa Fosfati (Phosphorus)
Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba.
Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye mashina na baadaye husambaa kwenye jani lote. Rangi inaonekana vizuri zaidi upande wa chini wa jani. Majani ya mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.

 

3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)
Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea kudumaa.
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi kama mahindi, mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye ncha. Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.

Manufaa ya matumizi ya mbolea
i). Kuongeza mavuno
ii). Ubora wa mazao
iii). Kuhifadhi rutuba ya udongo
iv). Kuongeza kipato kutokana na mavuno mengi na bora

Mambo muhimu ya kuzingatia
Ni muhimu kutumia mbolea za viwandani katika kilimo cha mahindi ili kumuwezesha mkulima kupata mavuno mengi. Lakini ikumbukwe kwamba matumizi ya mbolea ni lazima yaambatane na matumizi ya mbinu nyingine bora za kuzalisha mahindi, kama vile:
o   Kuandaa shamba
o   Matumizi ya mbegu bora
o   Kupalilia
o   Kupiga madawa ya kuzuia na kuua wadudu na magonjwa
o   Kuvuna kwa wakati unaostahili
o   Kuhifadhi vizuri mahindi


Mbolea za kukuzia mahindi
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:
  • UREA: 46% N
  • Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
  • Sulphate of Ammonia, SA: 21%

Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina magugu.
BOOSTER
Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu Mazao (kg 50/ekari = gramu 10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.
Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu. Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi hiki cha mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.
  • UREA:5gsawa na kizibo kimoja cha soda
  • CAN: 10g sawa na vizibo viwili vya soda
  • SA: 5g sawa na kizibo kimoja cha soda

PALIZI                                                                                                                                           Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba. . Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kungolea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES) hasa 2-4D.
Kilimo Mseto (mchanganyiko wa mahindi na mazao mengine)
Kilimo mseto (mchanganyiko) ni aina ya kilimo ambayo inajumuisha kupanda mazao mawili au zaidi kwenye shamba moja katika wakati mmoja. Aina hii ya kilimo inajumuishwa na kilimo hai au kilimo endelevu na inafanyika katika maeneo mengi. Katika kilimo mchanganyiko, zao moja huwa muhimu kwasababu za kiuchumi au chakula na zao jingine au mazao mengine hupandwa ili kusaidia hilo zao muhimu.
Dhumuni la kupanda mmea zaidi ya mmoja kwenye shamba ni kuongeza mavuno kutoka shambani kwa kutumia ardhi ambayo isingeweza kutumika yote kupanda mmea mmoja. Ni muhimu kufanya tathmini ya kina ili kuhakikisha kuwa mimea haitagombania maji, mwanga wa jua, nafasi ya kukulia na virutubisho vingine kutoka katika udongo.
Namna moja wapo ya kilimo mseto/mchanganyiko ni kupanda mmea wenye mizizi mirefu pamoja na mmea wenye mizizi mifupi au kupanda mmea mrefu wenye kuhitaji jua pamoja na mmea mfupi ambao hauhitaji sana jua. Hapa mmea mrefu utausaidia mmea mfupi kwa kuukinga na mwanga wa moja kwa moja kutoka kwenye jua. Miongoni mwa mazao ambayo yanaweza kupandwa pamoja na mahindi ni pamoja na Maharage, Njegere, karanga na Soya (jamii ya kunde).

MAGONJWA YA MAHINDI

i)                   Maize streak virus

Kudhibiti:
v  Mbegu bora inayostahimili ugonjwa,
v  kupanda mapema, kungoa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua vectors kama vile inzi weupe (white flies).Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.

iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi)



/Kudhibiti:
 Tumia mbegu zinazostahimili kuoza na mbegu kisasa au hybrid.

ii) Smut (Fugwe)
 
Dawa/Kudhibiti: Tumia dawa aina yaHelerat na ukifuata maagizo kamili ya namna ya kutumia.
Note magonjwa ya mahindi yapo mengi ila tumeandika machache kwa ufupi zaida ila kama utapata magonjwa tofauti na hayo hapo juu wasiana na wataalam wa kilimo kwa ushauri zaidi au pina +255717274387 kwa ushauri zaidi
WADUDU WAHARIBIFU
i) Stalk borer

Kudhibiti:
Tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
ii) Cutworms (Vikata Shina)

Kudhibiti:
Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili.
iii) Wanyama waharibifu


Kudhibiti:
 Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.
Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.


b) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer)

Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi
Kudhibiti:
Ø  Kuchanganya mahindi na mazao mengine kama vile mikunde,maharagwe
Ø  Kungoa mahindi yaliyoshambuliwa na kuyachoma moto
Ø  Tumia Sumu za asili kama vile maji ya mwarobaini
Ø  Tumia dawa za zviwandani kama Karate.
Ø   pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
a) Viwavi Jeshi

kudhibiti
  • Kuondoa vichaka karibu na shamba
  • Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
  • Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1L

Kuvuna
Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi
yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa.

Kukausha
Kama mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani.
Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi haijakauka vizuri.

Kusafisha & Kuhifadhi

Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa. Mahindi safi huchanganya na dawa za kuua wadudu kama vile Actellic Super ambayo ni vumbi nyeupe na kisha kuhifadhiwa kwenye ghala.

USHAURI:usilime kabda hujaa andaa soko usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.

 TEMBELEA MAKALA ZANGU KWENYE MTANDAO KANGETAKILIMO
·         Kilimo cha mihongo na mazao yote ya nafaka kama ufuta mbaazi ,choroko,mahindi ,,nk
·         Kilimo cha vitunguu,pilipli,nyanya,matikiti, na mazao yote ya mbogamboga
·         Kilimo cha matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
·         Ufugaji wa kuku  wa kienyeji kisasa

Note :Makala hii hutotelewa bure bila ya malipo na atakae kuuzia wasiliana nami 
  (kangetakilimo) +255717274387:
Whatsapp no: +255717274387:
email:emmanuelkangeta@gmail.com
Instagram :kangetakilimo
facebook : kangetakilimo
WEB:KANGETAKILIMO
                           AU andika katika google search engine KANGETAKILIMO


FREE MASTER PLAN AND COST BENEFIT  ANALYSIS(CBA)





No comments:

Post a Comment