Monday, August 21, 2017

KILIMO BORA CHA NYANYA NA KANGETAKILIMO



KILIMO BORA CHA NYANYA  NA  KANGETA KILIMO















 EMMANUEL KANGETA
tell:+255717274387
Whatsapp: +255717274387
email:emmanuelkangeta@gmail.com 
web:kangetakilimo 
fb :kangetakilimo
fb group:dondoo za kilimo
KILIMO BORA CHA NYANYA  (TOMATOES)
UTANGULIZI
 Nyanya ni zao ambalo hulimwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi ya TANZANIA na duniani kote. Asili yake ni kutoka Amerika ya kusini na kati. Nyanya ni miongoni mwa mazao jamii ya mboga mboga ambazo hulimwa na wakulima wengi. Tunda la nyanya hutumika kama kiungo muhimu katika mapishi na utengenezaji wa kachumbari na pia kama tunda. Nyanya ni chanzo kizuri cha vitamini mwilini na hutengeneza kipato kizuri kwa mkulima kama zikilimwa vizuri kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na uzalishaji. nyanya huhitajika zikiwa mbichi au zikiwa zimesindikwa(kangetakilimo)

 kutengeneza bidhaa nyinginezo kama vile nyanya za kopo na tomato sauce. na pia.Nyanya ni mmea wa sehemu za joto na hukua vizuri kwenye viwango vya joto baina nyuzi 18 hadi 24º Sentigredi.Mmea hunawiri kwenye udongo unaopitisha maji vizuri. Udongo unaonata haufai, kwani unahitaji umwagiaji wa maji wa hali ya juu.Udongo lazima ukaguliwe kama una chumvi au boroni nyingi au ukosefu wa madini mengineo.Mazao mazuri hupatikana kwenye udongo wenye uchachu (pH) wa 6.5. Uwe na mfumo wa kubadili mazao katika eneo kila mara ili kupunguza magugu, maradhi na ongezeko lawadudu.kangetakilimo
 

HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA NYANYA
 Kwa kawaida nyanya huhitaji hali ya hewa iliyotulia na kavu ili kuweza kufanya vizuri. Lakini nyanya humudu mazingira mengi. Mazingira yenye baridi kali au joto kali huharibu ukuaji pamoja na uzaaji wa nyanya. Udongo wowote wenye virutubisho hai unafaa kupandia nyanya kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa udongo unaweza kuupa mmea chakula kiasi kinachohitajika kukua na kuzaa. Matumizi ya maji yanatakiwa yaangiliwe vizuri ili kuhakikisha kuwa maji hayazidi wala kupungua kwani maji mengi husababisha mizizi kuoza, ni chanzo cha magonjwa na mmea kudumaa.(kangetakilimo)

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA NYANYA
Nyanya hupendelea udongo unaopitisha maji kwa urahisi na
wenye rutuba ya kutosha na hivyo hupenda Udongo
uwe umetifuliwa vya kutosha au matuta kuruhusu mizizi kushika vema.
AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
 unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi (Clay soil) –
 unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.
Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
• Tindikali ya udongo
• Kiasi cha mboji
• Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).

AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LA NYANYA
NYANYA hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia halinaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi (kangetakilimo)          
AINA ZA NYANYA
Kuna aina kuu mbili za nyanya kulingana na ukuaji wa mmea: yaani:
@ Nyanya ndevu (mfano Money maker)
@ Nyanya fupi zenye kutoa matawi mengi mfano Roma,Tanya na Cal J.
 

Figure kangetakilimo
Aina ya mbegu za nyanya
Kawaida


Chotara (Hybrid F1)
CAL - J
Bingwa F1
Moneymaker (Duara)
Kartik F1
Tanya
Asilia
Eden f1
KIASI CHA MBEGU
kwa ekari moja utahitaji Mbegu gram 100-150 kwa OPV variety, na Gram 30-50 kwa hybrid (F1) . Gharama za kutosha ekari moja kwa OPV variety ni tsh 100,000-180,000, na kwa Hybrid (F1) Gharama ni kati ya tsh 200,000-400,000 kutegemea na aina yenyewe ya mbegu na hekari. [
Vipimo kati ya mimea na mistari ni Sentimita 90 X 90
• Kupanda miche kwa karibu huleta mkusanyiko mkubwa wa majani, jambo linalochangia       kuzuka kwa maradhina kupunguza nguvu za dawa za kupuliza.
• Kwa zao nzuri na matunda bora tumia kipimo cha gramu 30 ya mbegu kwa ekari ili kufikia miche 9,000.




• Nyanya uathirika na kiwango kidogo cha unyevu nyevu. Maji ni muhimu wakati wa kutoa maua na kuanzakupatika kwa tunda. Ukosefu wa maji kunaweza kuliua tunda.(kangetakilimo)

UKUZAJI WA MICHE YA NYANYA
Miche ya nyanya huzalishwa kwenye kitalu kwa kupanda mbegu. Mbegu za nyanya huota baada ya siku 5 hadi 10.Baada ya kukua kitaluni kwa muda wa wiki 4 hadi 5 toka kuota kwa mbegu, miche hupandwa shambani. Kabla ya kupandikiza shambani miche huandaliwa kwa kupunguza umwagiliaji maji kwa siku moja au mbili ili miche izoee hali ngumu kabla ya kuhamishiwa shambani. Hapo shambani miche hupandikizwa kwa kuzamishwa katika kina kirefu zaidi ya ilivyo kuwa kitaluni. Hii inasaidia miche kutoa mizizi ya pembeni mingi zaidi kwa ajili ya kufyonza maji pamoja na virutubisho aridhini. Baada ya kupandikiza mwagilia maji yakutosha. Usimwagilie maji juu ya mche wa nyanya. Katika kipindi cha jua kali, tandaza nyasi kwenye tuta ili kupunguza upotevu wa maji na unaweza kuweka kivuli kwa kutumia majani ya miti au migomba. Kulingana na aina ya nyanya na rutuba ya udongo, nafasi ya kupandia ni sm 60 kati ya mstari hadi mstari na 45 hadi 60 nafasi ya mche hadi mche AU sm 90 kwa 50 AU 75 Kwa 40.  Kama udongo hauna rutuba ya kutosha inapendekezwa kutumia nafasi kubwa ya kupanda.
Utunzaji wa zao la nyanya  Nyanya fupi zisizo refuka kwenda juu, ni rahisi sana kutunza na
hazihitaji huduma nyingi. Tatizo kubwa ni kuwa kwa kutambaa chini, katika kipindi cha mvua huwa karibu na magonjwa yatokanayo na udongo. Katika kipindi cha jua kali, matunda huungua kwani mmea huwa na majani machache tu yanayo kinga matunda yasipigwe na mionzi ya jua.


MBOLEA
Licha ya mbolea ya kupandia, unashauriwa kuongeza mbolea kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche bustanini. Mbolea hii ya kukuzia iwekwe kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 hadi saba kutoka kwenye shina. Kwa mbolea kama vile CAN, NPK, au SA tumia kifuniko kimoja cha maji ya uhai kwa shina. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbilikabla ya mvuno wa kwanza.  Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine  yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, pilipili hoho, nk) inapaswa kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka. Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa nakuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya bustani (hasa usafi wa bustani na kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi yakuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya.  Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji egemezi,tunashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke. Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ilimwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Majani
yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche.  Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa
kadiri unavyo endelea kuvuna. Unashauriwa upunguze majani wakati wa asubuhi kwa kutumia mkono na pia usitoe zaidi ya majani matatu katika mmea kwa mara moja. kangetakilimo

KUPANDIKIZA
D.A.P. GRAMU 10 KWA KILA SHIMO
Changana na udongo na
mbolea ya samadi

WIKI MBILI BAADA YAKUPANDIKIZA


C.A.N. GRAMU 10 KWA KILA MMEA


Ndani ya shimo
Tandaza na kujaza

WIKI NNE HADI TANO BAADA YA
KUPANDIKIZA
N.P.K. 17;17:17 GRAMU 10 KWA KILA MMEA
Tandaza na kujaza
kangetakilimo

Namna ya kupandikiza miche kwenye Shambani/Bustanini
Ø  Panga kupandikiza miche shambani au bustanini siku ambayo jua siyo kali sana au wakati wa jioni wakati jua linakaribia kuzama.
Ø  Manyunyu ya mvua ni muhimu na husaidia sana wakati wa kupandikiza.
Ø  Shindilia udongo vizuri kuzunguka mizizi ya mche kwa kutumia vidole vyako ili kuufanya mche ujishike vizuri kwenye udongo.
Ø  Hakikisha unaweka nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea na mstari hadi mstari ili kuacha nafasi ya mizizi kutanukia na majani kuchanulia hapo baadaye.
Ø  Kama hamna mvua wakati wa kupandikiza inashauriwa kumwagilia hata kama mimea haionyeshi dalili za kukauka.
Ø  Ikinge mimea iliyopandikizwa na jua la moja kwa moja hadi wakati ambapo itaonyesha kuwa imeshika kwenye udongo, inaweza kukua yenyewe na kuhimili mwanga wa jua. 

UMWAGILIAJI WA NYANYA
Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi sana kwa ajili ya ukuaji wammea na matunda yake. Umwagiliaji uwe wa kulingana kwakila siku iliyo pangwa. Usibadilishe ovyo kiasi cha maji na ratiba ya kumwagilia. Hii inasababisha kuoza kwa kitako cha nyanya.Pia ili kutunza maji katika udongo, inashauriwa kuwekamatandazo katika mzunguko wa shina la nyanya au bustaniyote. Nyanya inayo kua vizuri hutumia maji lita mbili kwa siku
katika kipindi cha jua kali. Hivyo katika umwagiliaji ni busarakuzingatia kiasi hiki cha maji katika kipindi kama hiki. Pia kama unatumia keni, mpira au bomba usimwagilie maji juu ya matawi ya nyanya kwani umwagiliaji wa namna hii utasababishakuenea kwa magonjwa ya ukungu.kangetakilimo


MAGONJWA YA NYANYA

Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa
ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa.
Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na
mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.


Udhibiti
· Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa
zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.
· Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote
za pilipili na nyanya chungu.
· Tumia mbegu safi
· Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa

Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa
pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo
huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda
inayoshikana na kikonyo.kangetakilimo
Udhibiti
Ø  · Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
Ø  · Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna
Ø  · Tumia mbegu safi na bora








Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi
vinavyoishi kwenye udongo.
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.


Udhibiti
v  · Tumia mbegu safi na bora
v  · Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
v  · Teketeza masalia ya mimea
v  · Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu







Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo.
Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya
kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka
na kufa.


Udhibiti
v  · Panda mbegu safi
v  · Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,
             bilinganya au nyanya chungu
v  · Tumia mzunguko wa mazao
v  · Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye
               historia ya ugonjwa huu.
v  · Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu




Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na
ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda
mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya
imeshambuliwa na minyoo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa
husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na
kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea
kunyauka na kufa.

Udhibiti
*      · Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine
*      · Ondoa mabaki ya nyanya shambani
*      · Tumia mbegu bora na safi

Bakadoa (Bacterial spot)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia
kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia
huonekana kwenye majani na matunda.kangetakilimo


Udhibiti
· Panda mbegu bora na safi
· Tumia mzunguko wa mazao
· Teketeza masalia ya mazao
· Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo







Makovu bakteria (Bacterial canker)
Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani.
Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia
hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya
katikati.


Udhibiti
· Tumia mbegu bora na safi
· Teketeza masalia ya mazao
· Tumia mzunguko wa mazao









Rasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea
zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na
rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.

Udhibiti
· Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
· Ng’oa mimea yenye ugonjwa
· Tumia mzunguko wa mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi






Batobato (Tomato mosaic virus)
Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na
mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani
hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani
huwa linavinjikavunjika.


Udhibiti
· Tumia mbegu bora na safi
· Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
· Teketeza masalia ya mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi








WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha
matundu na hatimaye matunda huoza. 
Hupunguza ubora wa matunda.


Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.








Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa
wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha
majani kukauka.



Udhibiti
· Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,
Dursbarn na Thionex
· Mwagilia maji mara kwa mara
· Weka shamba katika hali ya usafi






Inzi weupe (White flies)
Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza
ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta.


Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.








Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na
kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa
matunda

Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.




 Minyoo (Nematodes)
Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi
hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na
kushindwa kuzaa


Udhibiti
· Tumia mzunguko wa mazao
· Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la
plastiki jeusi na nishati ya jua
· Choma masalia ya mazao
Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa
mchana hujificha kwenye udong
 Sota (Cutworms)
usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina
usawa wa udongo.
Udhibiti
· Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo
· Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.

Upungufu wa virutubisho aina ya chokaa. 
Dalili zake ni matunda ya nyanya kuoza sehemu ya kitako na
kuonyesha rangi nyeusi.
Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na utaratibu mzuri wa
kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo kiratiba na kiasi cha maji
yanayowekwa. Rutubisha mimea kwa madini ya chokaa kwa
kutumia mbolea aina ya CAN zenye madini haya.

UGONJWA WA UKOMA WA NYANYA
Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na inzi mweupe. Inzi
hawa hushambulia zaidi nyanya wa kati wa kiangazi, hasa
kipindi cha joto kali.

Dalili                         
• Majani machanga hujikunja na baadaye majani yote.
• Kupungua kwa utoaji maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo.
• Mmea kudumaa na kutozaa kabisa. Kuzuia Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika kupambana na mdudu huyo, yaani:
• Kuondoa mimea michache iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa huu kutoka mimea hii.
• Kutumia mbegu zilizo hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno mazuri.
• Usilime nyanya karibu na eneo lililo na mazao kama bamia,mipapai maana mimea hii huhifadhi inzi mweupe.
• Kuua inzi weupe wanaofyonza nyanya na kusambaza virusi kwa kutumia madawa. Tumia madawa kama vile Selecron, Decis, Karate n.k.
• Epuka kuchanganya zao la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile mipapai  na bamia.
• Ng'oa na kuchoma moto mimea yote iliyougua ugonjwa
huu.

Vidomozi
Vithiripi
Madhara ya vithiripi kwenye jani (1). Picha iliyokuzwa kuonyesha
kithiripi aliyekomaa (2). Madhara kwenye maua (3). Vithiripi
(4) na madhara yake kwenye matunda (5). Baadhi ya vithiripi
hueneza magonjwa ya virusi k.m. Tomato spotted wilt virus.

Kuvuna na baada ya kuvuna
Ø  Unapochagua madawa ya kunyunyiza nyanya ikishaanza kutoa matunda, zingatia muda wa kuvuna.
Ø  Kuwarithisha walaji na kupunguza kasi ya magonjwa, hakikisha matunda hayapati vidonda wakati wa kuvuna.
Ø  Hifadhi nyanya zilizovunwa kwenye kivuli ili zisikauke.
Ø  Kusanya masalia yote baada ya kuvuna na kuyachoma au kuyafukia ili kupunguza kasi ya kuzaliana wadudu
Ø  waharibifu na magonjwa ya nyanya.
Ø  Kuboresha rutuba ya udongo na kupunguza matatizo yatokanayo na udongo, usipende zao la nyanya mfulilizo.
Ø  Padilisha aina ya mazao mara kwa mara. Chagua aina ya mazao yasiyokuwa jamii ya nyanya kubadilisha, k.m.
Ø  kabechi, mahindi, maharagwe, vitunguu na majani ya mifugo.
 Note
Ikilazimu kunyunyiza dawa, tumia zilizosajiliwa kutumika kwenye nyanya tu. Fuata maelekezo ya
matumizi kinaganaga, zingatia muda wa kuvuna na njia salama za matumizi na kuhifadhi.

Wadudu Marafiki wa wakulima


Hifadhi marafiki wa wakulima
Ø Epuka au punguza matumizi ya madawa ya sumu kali, hasa yale yenye uwezo wa kuuwa
Ø wadudu wa aina nyingi wakiwemo marafiki wa mkulima. Ikilazimu kunyunyiza dawa, changua
Ø ile yenye madhara kidogo (k.m. Bt.) au yale ambayo hayatawadhuru marafiki wa mkulima (k.m.
Ø madawa yatokanayo na mwarubaini).
Ø Hifadhi mimea yenye kutoa maua kandokando ya bustani kuwapatia marafiki wa mkulima
Ø chakula aina ya nector na poleni.
Ø Endeleza kilimo cha mchanganyiko (mixed cropping). Mchanganyiko wa mimea unakuwa
Ø maficho na chakula cha marafiki wa mkulima.
Ø Matandazo yanachangia mazingira bora kwa marafiki wa mkulima waoishi katika udongo

MWISHO  WA MAKALA 
Free master plan and cost benefits analysis(CBA)        
             

USHAURI:usilime kabda hujaa andaa soko usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.

 TEMBELEA MAKALA ZANGU KWENYE MTANDAO KANGETAKILIMO
·         Kilimo cha mihongo na mazao yote ya nafaka kama ufuta mbaazi ,choroko,mahindi ,,nk
·         Kilimo cha vitunguu,pilipli,nyanya,matikiti, na mazao yote ya mbogamboga
·         Kilimo cha matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
·         Ufugaji wa kuku  wa kienyeji kisasa

Note :Makala hii hutotelewa bure bila ya malipo na atakae kuuzia wasiliana nami 
  (kangetakilimo) +255717274387:
Whatsapp no: +255717274387:
email: kangeta@gmail.com
Instagram :kangetakilimo
facebook : kangetakilimo
WEB:KANGETAKILIMO
                           AU andika katika google search engine KANGETAKILIMO
                       











No comments:

Post a Comment