EMMANUEL KANGETA
Tell:+255717274387
Whatsapp:
+255717274387
Email:emmanuelkangeta@gmail.com
or
Email:kangetakilimo@gmail.com
Web: kangetakilimo
Twitter:
kangetakilimo
Fb: kangetakilimo or emmanuelkangeta
KILIMO CHA BILINGANYA
Zao hili asili yake ni sehemu za nchi ya India nchi inayo ongoza dunia kwa
kilimo cha Bilinganya ni uchina hasa katika pwani za kusini mwa china inayo
lima asilima 59% duniani ikifuatiwa na India Uturuki,Misri Irani na Italy.`Bilinganya imo katika jamii ya mimea inayohusisha nyanya,
pilipili, viazi mviringo na nyanya mshumaa. Mboga hii ina viinilishe muhimu
kama vile madini aina ya chokaa na chuma, vitamini A, B hadi C, wanga, protni
na maji. Mboga hii hutumika kutengeneza supu au kama kiungo katika vyakula
mbalimbali. Vile vite huweza kuhifadhiwa kwa kukatakata vipande na kuwekwa
kwenye makopo. Zao hili huhitaji hali yajoto la wastani, udongo wenye kina
kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya
hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini katika nchi za Kitropild
(joto) zao hili hulimwa kwa msimu mmoja. Zao
hili huhitaji haliyahewa ya joto hu
AINA ZA BILINGANYA:
Kuna Aina za bilinganya zinazolimwa
kwa wingi katika nchi za ukanda wajoto ni kama zifuatazo:-
ü Black Beauty:
Aina hii huzaa sana, matunda yake
meusi, makubwa, na ya mviringo.
Aina ya Bilinganya Black Beauty
ü Florida Market
Matunda ya Florida Market yana umbo Kama yai. Aina hii pia
huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa wa mnyauko bakiteria
(Bacterial wilt).
ü Florida High Bush
Matunda yake ni makubwa ycnye umbo la yai na rangi ya kijani
kibichi iliyochanganyika na nyeusi.
ü
NewyorkSpineless
Matunda ya
Newyork Spineless ni ya mviringo, makubwa na yana rangi ya zambar
au.
-
ü Peredeniya
Aina hii huzaa sana, matunda yake ni
makubwa kiasi na yana umbo la yai.
Aina
zingine za bilinganya ni
Matale, Kopek na
Rosita.
Aina hizi huvumilia sana
mashambulizi ya ugonjwa wa mnyauko bakteriaf
JINSI YA KUANDAA KITALU
Kitalu ni sehemu maalumu
iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya kuipeleka shambani
ama bustanini. Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji
vitalu. Mimea Kama bilinganya.Mimea ambayo inachelewa kuchipua, kukua, na yenye
kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga inashauriwa
ipandwe kwanza kwenye kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha
kupandikizwa bustanini au shambani. Weka udongo debe mbili, mbolea debe moja na
makapi ya mpunga ama mchanga debe moja (2:1:1). Changanya vizuri kwa kutumia
koleo na utandaze huo mchanganyiko kwa kutumiaa reki. Panda au sia mbegu bora
ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, ambazo hazijashambuliwa na magonjwa au
wadudu na zenye uwezo wa kuota vizuri zikipandwa. Kama unahitaji kununua mbegu
inashauriwa kununua
mbegu kutoka kwa mawakala
wanaoaminika. Unaweza kupanda kwa mstari ama kwa kusia. Miche ikiwa tayari
ikapandwe bustanini wakati wa jioni na imwagiliwe vizuri. Bustani iwe
imeandaliwa kabla ya siku ya kuhamisha miche.
Gramu 500 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo
la hekta moja. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina
kiwe sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu fukia na tandaza nyasi kavu na kisha
mwagilia maji. Endelea kumwagilia kitalu kila siku, asubuhi na jioni, hadi
mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku ya 10 hadi 12.Udongo
kwenye kitalu unatakiwa uwe unaweza kupitisha maji vizuri. Tayarisha kitalu
chako kwa kuchimba au kulima udongo angalau 30 sm kwenda chini, ondoa mabaki
yoyote ya mimea na mizizi na vunja mabonge yote ya udongo kisha changanya
samadi iliyooza vizuri au mboji iliyoiva vizuri. Sawazisha vizuri na reki hadi
udongo uwe vizuri.
Pima upana na urefu wa kitalu
ambao utakuwezesha kufikia kila pembe ya kitalu kwa urahisi bila kukanyaga
ndani ya kitalu. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kuleta magonjwa kwenye
kitalu na itarahisisha kungoa magugu pamoja na kuhamisha miche kwenda shambani.
Kama unasia mbegu katika
mistari hakikisha kuwa mistari ipo katika umbali Baada ya kusia mbegu funikia na udongo kidogo
kutegemea na ukubwa wa mbegu. Siku moja kabla ya kusia mbegu, mwagia kitalu
maji hadi kilowe vizuri. Kwa siku zinazofuata inashauriwa kumwagilia maji
kidogo kidogo hadi pale zitaka
Sifa za sehemu nzuri ya kutengeneza kitalu
Karibu na chanzo cha maji au bomba.
Sio mbali na shambani/bustanini.
Mbali na wanyama ama kuwe na
uzio.
Pasiwe na upepo mkali
Iwe na kivuli.
Iwe karibu na njia
kurahisisha usafirishaji pindi ikibidi.
Matunzo ya kitalu
Baada ya kusia mbegu hakikisha
kitalu hakipati jua la moja kwa moja na mvua kubwa. Weka matandazo ya majani
ili kusaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu na kuweza kuzuia mwangaza wa jua wa
moja kwa moja.
Angalizo:
Ondoa matandazo mara tu mbegu zitakapochipua
Ruhusu kivuli kidogo kwenye miche na usiweke kivuli kikubwa sana kwani
kitaifaya miche isikue
Baada ya kuchipua mwagilia maji taratibu kwa kutumia bomba au chupa yenye
vitundu vidogo dogo. Hakikisha maji hayazidi kwenye kitalu kwani yanaweza
kusababisha ugonjwa na miche kuharibika.
Hakikisha kitalu ni kisafi wakati wote. Ondoa magugu yoyote yatakayojitokeza.
Punguzia miche kama imejazana sana ili kuipa nafasi ya kukua vizuri.
Kagua kitalu mara kwa mara
kuangalia kama kuna uvamizi wowote wa wadudu waharibifu au mlipuko wa ugonjwa.
Baada ya miche yako kufikia
muda wa kupandikiza inashauriwa kuchagua miche yenye afya nzuri ambayo haijaathirika
na wadudu wala kuwa na dalili yoyote ya ugonjwa.
Mwagilia maji kwenye kitalu
usiku mmoja kabla ya siku ya kung’oa ili kurahisiha ung’oaji na kuzuia
uwezekano wa mizizi kuharibika. Hakikisha miche iliyong’olewa haipati jua la
moja kwa moja au hewa yenye joto. Inashauriwa kuiweka kwenye trei au kikapu na
kuifunika na majani au nguo mbichi wakati inapelekwa shambani au bustanini.
Namna ya kupandikiza miche kwenye Shambani/Bustanini
Panga kupandikiza miche shambani au bustanini siku ambayo jua siyo kali sana au
wakati wa jioni wakati jua linakaribia kuzama.
Manyunyu ya mvua ni muhimu na husaidia sana wakati wa kupandikiza.
Shindilia udongo vizuri kuzunguka mizizi ya mche kwa kutumia vidole vyako ili
kuufanya mche ujishike vizuri kwenye udongo.
Hakikisha unaweka nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea na mstari hadi mstari
ili kuacha nafasi ya mizizi kutanukia na majani kuchanulia hapo baadaye.
Kama hamna mvua wakati wa kupandikiza inashauriwa kumwagilia hata kama mimea
haionyeshi dalili za kukauka.
Ikinge mimea iliyopandikizwa
na jua la moja kwa moja hadi wakati ambapo itaonyesha kuwa imeshika kwenye
udongo, inaweza kukua yenyewe na kuhimili mwanga wa jua.
Faida za Kitalu
cha miche kwa mkulima
Kuchagua miche iliyo na afya nzuri.
Kuthibiti magugu shambani kabla hajahamishia miche shambani.
Kupata miche ya kupanda muda wowote atakao.
Ni rahisi kuthibiti vijidudu
viharibifu na magonjwa kwenye kitalu kuliko shambani ama bustanini. Hii ni kwa
sababu kitalu kinakua na miche mingi na
KUHAMISHA MICHE YA BILINGANYA KATIKA KITALU
Miche
huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki sita hadi nane. Wakati huu
huwa na urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (sawa na urefu wa kalamu ya risasi).
Mwezi
mmoja kabla kupanda miche, rutubisha udongo kwa kuweka mbolea za asili
zilizooza vizuri. Mbolea hizi ni kama samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.
Weka
kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka ndoo moja
hadi mbili zenye ujazo wa lita 20 katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya
mchanganyiko aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye shimo wakati
wa kupandikiza mche. Kiasi kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na
nusu kijiko mpaka kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.
Nafasi
ya kupandikiza hutegemea aina ya bilinganya. Aina ndogo hupandikizwa katika
nafasi ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 50
mpaka 60 kutoka mche hadi mche. Aina kubwa hupandikizwa katika nafasi nafasi ya
sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 80 mpaka 90
kutoka mche hadi mche. Kazi ya kuhamisha miche ifanyike kwa uangalifu mkubwa
ili kuepuka kuikata mizizi.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH kiwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH kiwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na
unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji
na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi
(Clay soil) –
unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji
wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.
Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba
ya udongo ni:
• Tindikali ya udongo
• Kiasi cha mboji
• Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na
Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.
Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo.
Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko
7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa
kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya
tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).
bilinganya
hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza
kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili
ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.
Matandazo (Mulches)
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
Palizi
Hakikisha
shamba ni safi wakati wote ili kuzuia ushindani wa chakula, maji na mwanga kati
ya mimea na magugu. Usafi wa shamba pia huondoa maficho ya wadudu waharibifu na
huzuia kuenea kwa magonjwa
MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho
mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye
mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati
na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium,
boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili,
yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na
kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.
Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic
fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or
industrial fertilizers)
Mbolea Za Asili (Organic
Fertilizers)
Hizi
ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili
ni kama vile:
i.
Mbolea vunde:
inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana
na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii.
Samadi:
kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na
ndege.
iii.
Mbolea za kijani:
hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
iv.
Majivu:
ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa
wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v.
Matandazo
(mulch):
ambayo
baadaye yakioza huwa mbolea.
Mbolea
Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa
viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum
vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa
lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho
vinavyohitajika na mimea.
Mbolea Za Kupandia
Mbolea maarufu za kupandia katika
soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao. Lakini
zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa ‘Kukuza matumizi ya Minjingu
Phosphate’ ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.
1. Diammonium Phosphate (DAP)
Ina virutubisho viwili - naitrojeni
ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 18, na fosfati (P2O5) ambacho kiko kwa
kiwango cha asilimia 46. Inapatikana katika hali ya chengachenga (granules).
2. Minjingu Phosphate
Ina kiwango cha fosfati (P2O5) asilimia 29 na inatumika
zaidi kwa kutoa kirutubisho hiki. Lakini inaongeza vilevile kirutubisho cha
chokaa (calcium) ambacho kipo kwa kiwango cha asilimia 40. Chokaa inasaidia
vilevile kukabili tindikali (acidity) ya udongo.
3. Minjingu Mazao
Hii ni mbolea mpya inayotokana na Minjingu Phosphate lakini
imeongezwa virutubisho vingine vitano ambavyo ni naitrojeni (10%), salfa (5%),
zinki (0.5%), shaba (0.5%), boroni (0.1%), pamoja na chokaa (25% CaO) na
magnesium (1.5% MgO). Virutubisho vilivyoongezwa hususani naitrojeni na salfa
ni vile ambavyo vinakosekana katika aina nyingi za udongo.
Zinki, shaba na boroni vimeongezwa kwa tahadhari kwa sababu
vinaonyesha dalili za upungufu katika baadhi ya maeneo. Minjingu Mazao iko
katika hali ya chengachenga.
namna ya kuchagua mbolea ya
kupandia
Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao
zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya
6.2 ili mbolea za Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye
tindikali zaidi ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa
potashi, tumia mbolea zinazorejesha madini hayo.
Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza
mazao. Mboji huwa haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji
husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya
kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha
mbolea na mbegu).
1. Upungufu Wa Naitrojeni (Nitrogen)
Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo,
na mwishowe hutoa mazao kidogo . Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza
usitoe mazao. Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha mmea
kudumaa. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea
kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa sana, majani hugeuka rangi ya njano kutoka
pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza kugeuka.Majani ya mwanzo hukauka mapema
kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha.
2. Upungufu Wa Fosfati (Phosphorus)
Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina
kuwa membamba. Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi
hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye mashina na baadaye husambaa kwenye
jani lote. Rangi inaonekana vizuri zaidi upande wa chini wa jani. Majani ya
mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye mimea yenye upungufu
kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.
3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)
Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea
kudumaa.
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho
kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi
, mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na
kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye
ncha.}UYR$%Y#@ u
nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo
hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.
JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUPANDA BILINGANYA
Mbolea hizi ni
kama samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.Weka kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa
hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita 20
katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K yenye
uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi
kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka kijiko
kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.
JINSI YA
KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUKUZIA BILINGANYA
Mbolea
ya kukuzia aina ya CAN au S/A huwekwa wiki tatu baada ya mmea kuanza kutoa
maua. Weka kiasi cha kizibo kimoja cha soda kuzungukia kila mche. Mbolea iwekwe
katika umbali wa sentimita tano kutoka kwenye shina. Hakikisha mmea haugusi
mche.
Kukata kikonyo(kilele)
Wiki mbili baada
ya kupandikiza miche, kata sehemu ya juu ya mmea (kilele) kama umepanda aina
ndefu ya bilinganya. Hii itasaidia kupata matawi matatu hadi manne na mmea
kutengeneza kupata matawi matatu hadi manne na mmmea kutengeneza umbile la
kichaka. Matawi yakizidi manne yaondolewe ili kupata mazao mengi na bora.
umwagiliaji wa bilinganya
Zao
la bilinganya hustawi vizuri likipata maji ya kutosha kwasababu asili ya zao
hili ni maji. Umwagiliaji ufanyike kila siku asubuhi na jioni kutegemea hali ya
hewa ya sehemu husika.
KUVUNA
Bilinganya huanza kutoa matunda
yaliyokomaa baada ya miezi miwili hadi mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji
huendelea kwa muda wa zaidi ya miezi minne na hauna budi ufanyike mapema mara
tu matunda yanapokomaa. Matunda yaliyo komaa sana hayafai kuliwa kwa sababu
huwa na kambakamba na mbegu zilizokomaa. Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa
kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.Kwa kawaida zao hili huzaa sana
iwapo limetunzwa vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri linaweza kutoa mavuno tani
50 hadi 60 kwa hekta. Hata hivyo mavuno mengi hutegemea aina ya bilinganya,
umwagiliaji na rutuba ya udongo.
WADUDUWAHARIBIFU:
Ø Vinyatomvu wa Bilinganya (Eggplant Lacebugs):
Wadudu hawa hushambulia zaidi sehemu
ya chini ya jani. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha majani kuwa na
mabaka meupe au njano.
Mashambulizi yakizidi majani huanguka chini.
Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa kwa kunyunyizia moja ya dawa zifuatazo:-
Deltamethrin (Decis), Dimethoate
(Sapa Dimethoate) Fenvalerate (Sumicidin), Lambda - Cyhalothrin (Karate).
Ø Vidukari au Wadudu mafuta (Cotton Aphids):
Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi. Hushambulia majani
machanga na kuyasababisha kudumaa na kukunjamana.
Zuia wadudu hawa kwa kutumia mojawapo ya dawa zifuatazo:-
Dimecron 50% E.C, Lambda - Cyhalothrin (Karate) Dichlorvos (Nogos).
Ø
Utiriri wa Mimea (Red Spider Mites):
Ni vidudu vidogo vyenye rangi
nyekundu iliyoiva. Hushambulia majani kwa kufyonza utomvu. Majani
yaliyoshambuliwa huonyesha utando kama wa buibui.
Mashambulizi yakizidi mmea hudumaa,
majani hukauka na hatimaye hufa. Utiriri unazuiwa kwa kutumia dawa zifuatazo:-
Acrex, Karathane 25% W.P., Dimethoate, Ekalux, Kelthane.
Ø
Minyoo Fundo (Root knot nematodes):
Wadudu hawa hushambulia mizizi.
Hutoa kinyesi ambacho ni sumukwammea. Sumu hii husababisba mizizi kuwa na nundu
kama ya mizizi ya maharagwe.
Mashambalizi yakizidi mmea hudumaa,
hunyauka na hatimaye hufa. Njia ya kuzuia wadudu hawa ni kubadilisha mazao. Kwa
mfano; baada ya kuvuna zao hili, zao linalofuata lisiwe lajamii moja na
bilinganya, kamavile nyanya, pilipili naviazi mviringo. Pia dawa aina ya
Carbofuran (Furadan) inaweza kutumika.
MAGONJWA:
ü Mnyauko
Bakteria (Bacterial Wilt):
Ugonjwa huu husababishwa na
backteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wajua kali
Mnyauko bakteria unaweza kuzuiwa kwa
kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la
bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano.
Njia nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile Matale, Kopek, na
Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.
ü Phomopsis
Vexans:
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria na hushambulia majani,
shina na matunda.
ü
Verticillium Wilt:
Huenezwa na maji na husababisha mmea kudumaa, majani
kukunjamana na kuanguka.
Magonjwa ya Phomopsis Vexans na
Verticillium Wilt yanaweza kuzuiwa kwa kung'oa na kuchoma moto mimea
iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao, na kuweka shamba katika hali ya usafi
wakati wote.
Karibu sana shambani
MWISHO WA MAKALA
Hemed Emmanuel Kangeta
TEMBELEA MAKALA
ZANGU KWENYE MTANDAO KANGETAKILIMO
·
Kilimo cha
mihongo na mazao yote ya nafaka kama ufuta mbaazi ,choroko,mahindi ,karanga,nk
·
Kilimo cha
vitunguu,pilipli,nyanya na mazao yote ya mbogamboga
·
Kilimo cha
matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
·
Ufugaji wa
kuku wa kienyeji kisasa
Note
Makala hii hutotelewa bure bila ya
malipo na atakae kuuzia wasiliana nami
(kangetakilimo)
+255717274387:
Whatsapp no: + 255717274387:
email: emmanuelkangeta@gmail.com
Instagram :kangetakilimo
facebook : kangetakilimo
WEB:KANGETAKILIMO
AU andika katika
google search engine KANGETAKILIMO
No comments:
Post a Comment