Sunday, April 29, 2018

KILIMO BORA CHA VITUNGUU SWAUMU NA KANGETA KILIMO



KILIMO CHA VITUNGUU SWAUMU
Vitunguu swaumu hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya ubaridi wastani Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na, ASIA. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Nchini Tanzania, vitunguu hulimwa kwenye mikoa ya Iringa,Morogoro ,mkoani Arusha, Babati,Kilimanjaro, na Morogoro na baadhiya sehemu za Mkoa wa ya tanzania,



UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA VITUNGUU SWAUMU
Mahitaji ya udongo na mbolea ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mmea wowote ule, hata hivo mahitaji hayo hutofautiana kati ya mmea moja na mwingine kutokana na kutofautiana kwa sehemu ya zao katika hiyo mimea (yaani economic part of a plant). Kwa mfano: VITUNGUU. Udongo una rutuba ya asili yaani virutubisho katika udongo, mboji (organic fertilizer), na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye udongo. Rutuba ya udongo inategemea sana hali ya udongo kikemia, kibiolojia na kifizikia.


AINA ZA UDONGO
Kuna aina tatu ya udongo ambazo ni
 1)Kichanga (Sand soil)
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.


 2)Tifutifu (Loam soil)

unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.

3)Mfinyanzi (Clay soil)
unahifahdi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mdogo.


Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
 Tindikali ya udongo
 Kiasi cha mboji
 Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.



SOIL PH
pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0). vitunguu swumu hustawi kwenye udongo wa tifutifu wenye tindikali ya wastani na virutubisho vya kutosha.


UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA VITUNGUU
Hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH ya 6 hadi 7.hukubali katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.unaweza kulima katika udongo wa kichanga au mfinyanzi japokuwa katika udongo wa mfinyazi kama mvua itakuwa kubwa na maji yakatuama kwa muda mrefu huzuia ukuaji mzuri wa ila kitunguuswumu hufanya vizuri sana katika udongo mfinyanzi tifutifu.

MAANDALIZI YA SHAMBA LA VITUNGUU
Taarisha shamba lako la VITUNGUU mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Magonjwa kama yale ya majani hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu.Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
1. Jembe la mkono - wengi wanatumia
2. Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
3. Power tillers
4. trekta


HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA VITUNGUU
Hali ya hewa inayofaa ni ile ya ubaridi wastani. Joto linalohitajika ni kati ya nyuzi joto 14°C hadi 27°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 25°C. Joto la juu hufanikisha utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji .Pia zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa vitunguu. Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi unyevu kama vile udongo wa mfinyanzi tifutifu. mwezi machi hadi mei kutegemea na msimu wa kilimo. Hivyo kilimo hiki hufanyika mara baada ya mvua za masika kubwa kuisha. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri

MBEGU ZA VITUNGUU
Kuna aina Kama mbili za mbegu za vitunguu (bulbs)
1) Mbegu aina ya chotara (hybrid)
3) Mbegu aina ya composite (asili)
Zingatia Kitunguu swaumu hupandwa "BULB" na sio mbegu kama vitunguu maji. Ni ile punje ambayo imekuwa na kukomaa vizuri na isyoathiliwa na magonjwa


Ushauri

matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya
Mwinuko kutoka usawa wa bahari
 Kiasi cha mvua katika eneo husika
 Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa


AINA ZA VITUNGUU SWAUMU

Vitunguu swaumu vipo vya aina tatu za vitunguu nazo ni
I) Antichoke
Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea

ii) Soft neck
Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani

iii) Silver skin
Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

JINSI YA KUANDAA KITALU VITUNGUU

Hapa Tanzania upandaji wa mbegu za vitunguu katika kitalu kwa ujumla huanza mwezi machi hadi mei kutegemea na msimu wa kilimo ingawa sio lazima. Hivyo kilimo hiki hufanyika mara baada ya mvua za masika kubwa kuisha. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vitunguu.Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika tuta la kitalu. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari.Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota.



matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga. Mbegu huota baadaya siku 7 hadi 10.Kitalu ni sehemu maalumu iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya kuipeleka shambani ama bustanini. Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji vitalu. Mimea Kama vitunguu.Mimea ambayo inachelewa kuchipua, kukua, na yenye kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga inashauriwa ipandwe kwanza kwenye
kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha kupandikizwa bustanini au shambani. Weka udongo debe mbili, mbolea debe moja na makapi ya mpunga ama mchanga debe moja (2:1:1). Changanya vizuri kwa kutumia koleo na utandaze huo mchanganyiko kwa kutumiaa reki. Panda au sia mbegu bora ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, ambazo hazijashambuliwa na magonjwa au wadudu na zenye uwezo wa kuota vizuri zikipandwa. Kama unahitaji kununua mbegu inashauriwa kununua


mbegu kutoka kwa mawakala wanaoaminika. Unaweza kupanda kwa mstari ama kwa kusia. Miche ikiwa tayari ikapandwe bustanini wakati wa jioni na imwagiliwe vizuri. Bustani iwe imeandaliwa kabla ya siku ya kuhamisha miche. Kilo 200 hadi 300 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo la hekta moja. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina kiwe sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu fukia na tandaza nyasi kavu na kisha mwagilia maji. Endelea kumwagilia kitalu kila siku, asubuhi na jioni, hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku ya 6 hadi 10..Udongo kwenye kitalu unatakiwa uwe unaweza kupitisha maji vizuri. Tayarisha kitalu chako kwa kuchimba au kulima udongo angalau 30 sm kwenda chini, ondoa mabaki yoyote ya mimea na mizizi na vunja mabonge yote ya udongo kisha changanya samadi iliyooza vizuri au mboji iliyoiva vizuri. Sawazisha vizuri na reki hadi udongo uwe vizuri.


Pima upana na urefu wa kitalu ambao utakuwezesha kufikia kila pembe ya kitalu kwa urahisi bila kukanyaga ndani ya kitalu. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kuleta magonjwa kwenye kitalu na itarahisisha kungoa magugu pamoja na kuhamisha miche kwenda shambani. Kama unasia mbegu katika mistari hakikisha kuwa mistari ipo katika umbali Baada ya kusia mbegu funikia na udongo kidogo kutegemea na ukubwa wa mbegu. Siku moja kabla ya kusia mbegu, mwagia kitalu maji hadi kilowe vizuri. Kwa siku zinazofuata inashauriwa kumwagilia maji kidogo kidogo hadi pale zitaka


Sifa za sehemu nzuri ya kutengeneza kitalu
 Karibu na chanzo cha maji au bomba.
 Sio mbali na shambani/bustanini.
 Mbali na wanyama ama kuwe na uzio.
 Pasiwe na upepo mkali
 Iwe na kivuli.
 Iwe karibu na njia kurahisisha usafirishaji pindi ikibidi.


Matunzo ya kitalu

Baada ya kusia mbegu hakikisha kitalu hakipati jua la moja kwa moja na mvua kubwa. Weka matandazo ya majani ili kusaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu na kuweza kuzuia mwangaza wa jua wa moja kwa moja.
Angalizo:
Ondoa matandazo mara tu mbegu zitakapochipua
Ruhusu kivuli kidogo kwenye miche na usiweke kivuli kikubwa sana kwani kitaifaya miche isikue


Baada ya kuchipua mwagilia maji taratibu kwa kutumia bomba au chupa yenye vitundu vidogo dogo. Hakikisha maji hayazidi kwenye kitalu kwani yanaweza kusababisha ugonjwa na miche kuharibika.


Hakikisha kitalu ni kisafi wakati wote. Ondoa magugu yoyote yatakayojitokeza.
Punguzia miche kama imejazana sana ili kuipa nafasi ya kukua vizuri.
Kagua kitalu mara kwa mara kuangalia kama kuna uvamizi wowote wa wadudu waharibifu au mlipuko wa ugonjwa.


Baada ya miche yako kufikia muda wa kupandikiza inashauriwa kuchagua miche yenye afya nzuri ambayo haijaathirika na wadudu wala kuwa na dalili yoyote ya ugonjwa.
Mwagilia maji kwenye kitalu siku mmoja kabla ya siku ya kung’oa ili kurahisiha ung’oaji na kuzuia uwezekano wa mizizi kuharibika. Hakikisha miche iliyong’olewa haipati jua la moja kwa moja au hewa yenye joto. Inashauriwa kuiweka kwenye trei au kikapu na kuifunika na majani au nguo mbichi wakati inapelekwa shambani au bustanini.
Namna ya kupandikiza miche kwenye Shambani/Bustanini.Panga kupandikiza miche shambani au bustanini siku ambayo jua siyo kali sana au wakati wa jioni wakati jua linakaribia kuzama.Manyunyu ya mvua ni muhimu na husaidia sana wakati wa kupandikiza.Shindilia udongo vizuri kuzunguka mizizi ya mche kwa kutumia vidole vyako ili kuufanya mche ujishike vizuri kwenye udongo.Hakikisha unaweka nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea na mstari hadi mstari ili kuacha nafasi ya mizizi kutanukia na majani kuchanulia hapo baadaye.Kama hamna mvua wakati wa kupandikiza inashauriwa kumwagilia hata kama mimea haionyeshi dalili za kukauka.Ikinge mimea iliyopandikizwa na jua la moja kwa moja hadi wakati ambapo itaonyesha kuwa imeshika kwenye udongo, inaweza kukua yenyewe na kuhimili mwanga wa jua.


Faida za Kitalu cha miche kwa mkulima

o Kuchagua miche iliyo na afya nzuri.
o Kuthibiti magugu shambani kabla hajahamishia miche shambani.
o Kupata miche ya kupanda muda wowote atakao.
o Ni rahisi kuthibiti vijidudu viharibifu na magonjwa kwenye kitalu kuliko shambani ama bustanini. Hii ni kwa sababu kitalu kinakua na miche mingi na JINSI YA UPANDAJI Tifua udongo kidogo kisha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa mimea tu. Tengeneza tuta za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa mbolea Inashauliwa usitumie NPK.Tabia ya Mmea ya Vitunguu swaumu hufanya vizuri kipindi cha baridi kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August,Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 . Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.


MBOLEA

Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.
Aina za mbolea


Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)


Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile:
i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii. Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
iii. Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
iv. Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v. Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.


Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.


Mbolea Za Kupandia kitunguu
Mbolea maarufu za kupandia katika soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao. Lakini zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa ‘Kukuza matumizi ya Minjingu Phosphate’ ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.
Jinsi ya kuchagua mbolea ya kupandia
Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya 6.2 ili mbolea za Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye tindikali zaidi ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa potashi, tumia mbolea zinazorejesha madini hayo. Kwa kwa kitunguu pandia TSP.


Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza mazao. Mboji huwa haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha mbolea na mbegu).
Dalili Ya Upungufu Wa Virutubisho Mbalimbali


1. Upungufu Wa Naitrojeni (Nitrogen)
Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo, na mwishowe hutoa mazao kidogo . Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza usitoe kabisa.
Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha mmea kudumaa. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa sana, majani hugeuka rangi ya njano kutoka pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza kugeuka. Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha


2. Upungufu Wa Fosfati (Phosphorus)
Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba.
Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye mashina na baadaye husambaa kwenye jani lote. Rangi inaonekana vizuri zaidi upande wa chini wa jani. Majani ya mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.


3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)
Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea kudumaa.
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi kama mahindi, mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye ncha. Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.
Manufaa ya matumizi ya mbolea
i). Kuongeza mavuno
ii). Ubora wa mazao
iii). Kuhifadhi rutuba ya udongo
iv). Kuongeza kipato kutokana na mavuno mengi na bora
Mambo muhimu ya kuzingatia
Ni muhimu kutumia mbolea za viwandani katika kilimo cha VITUNGUU ili kumuwezesha mkulima kupata mavuno mengi. Lakini ikumbukwe kwamba matumizi ya mbolea ni lazima yaambatane na matumizi ya mbinu nyingine bora za kuzalisha, kama vile:
o Kuandaa shamba
o Matumizi ya mbegu bora
o Kupalilia
o Kupiga madawa ya kuzuia na kuua wadudu na magonjwa
o Kuvuna kwa wakati unaostahili
o Kuhifadhi vizuri
Mbolea za kukuzia vitunguu swaumu
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:
 UREA: 46% N
 Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
 Sulphate of Ammonia, SA: 21%
Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina magugu.BOOSTER


Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 2, kwa mara 2-3 mpaka kitunguu kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yuko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.


Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu. Kwenye mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada yakuhamisha mimea kwenye kitalu. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi kwa njia ya kusia mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua vitunguu ni mrefu ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.



PALIZI

Katika kilimo cha vitunguu, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha vitunguu shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kung’olea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES).kama vile ROUNDUP MAGONJWA & WADUDU

WADUDU
Wadudu wanaosababisha uharibifu mkubwa kwenye vitunguu ni chawa wekundu (thrips) na sota (cutworms). Wadudu wengine ni pamoja na utitiri wekundu (red spider mites) na vipekecha majani (leaf miner)


1) Wadudu chawa (thrips)
Uharibifu uletwao na wadudu chawa, unatofautiana msimu mmoja na mwingine kutegemeana na hali ya hewa. Mvua kidogo pamoja na joto kali unasababisha mlipuko wa wadudu. Wanshambulia majani kwa kukwaruakwarua na kunyonya maji hivyo kusababisha majani kuwa na rangi ya fedha/siliver na baadaye majani yanakauka. Upungufu mkubwa wa mazao unatokea. Wadudu chawa (thrips) kwenye majani ya vitunguu



Njia ya kudhibiti hawa wadudu
· Kuweka shamba katika hali ya usafi
· Kuondoa magugu shambani na yanayozunguka shamba la vitunguu
· Kupulizia dawa ya wadudu kama karate, selecron, dursban, actellic.


2) Sota (Cutworms)
Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.

Jinsi ya kudhibiti
Tumia dawa Kama Karate Dursban na Actellic ,duduba,duduall
Kuweka shamba katika hali ya usafi zaid

3) Utitiri wekundu (Red spider mites)
Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.
Njia ya kudhibiti:
· Kupulizia dawa za wadudu Karate na Selecron.
· Kuteketeza masalia ya mazao

· Kutumia mzunguko wa mazao


MAGONJWA

a) Baka zambarau (Puple Blotch)
Ungonjwa huu unasababishwa na kuvu (fangasi). Chanzo kikubwa cha ugonjwa ni mbegu zenye ugonjwa. Pia ugonjwa unajitokeza wakati kuna ukungu na unyevunyegu mwingi hewani has wakati wa masika. Kiasi cha 60-80 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa
hautadhibitiwa. Dalili za ugonjwa ni:- · Kujitokeza madoa meupe yaliyodidimia kwenye majani na kwenye mashina ya mbegu · Rangi ya zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe. · Majani kuanguka · Mashina ya mbegu kuanguka kabla ya mbegu kutengenezwa



Njia za kudhibiti:-
· Kupanda mbegu safi
· Kupanda vitunguu kwa kutumia mzunguko wa mazao
· Kuteketeza msalii ya vitunguu baada ya kuvuna
· Kupulizia dawa zilizopendekezwa kama Dithane M45 na Ridomil MZ. Dawa hizi zinachanganywa na supergrow ili zisijishike kwenye majani.


b) Ubwiri vinyoya (Downy Mildew)

Ugonjwa huu unasababishwa na kuvu (fangasi) na kuenezwa na mbegu, hewa na masalia ya vitunguu. Unajitokeza wakati kuna unyevunyevu mwingi hewani hasa wakati wa masika na dalili zake ni kama zifuatazo:-
· Madoa yenye umbo la yai, rangi ya njano iliyofifia hujitokeza kwenye majani makukuu na kusambaa mpaka kwenye majani machanga.
· Baada ya siku chache madoa ya njano yanafunikwa na ukungu wa rangi ya kijivu.
· Majani yanasinyaa na kufa kuanzia kwenye ncha.
· Shina la mbegu huzungukwa na vidonda na kusababisha kichwa cha mbegu kuanguka.


Njia za kudhibiti ugonjwa ni kama zifuatavyo:-
· Kupanda mbegu safi
· Kupanda vitunguu kufuata mzunguko wa mazao
· Kupulizia dawa za ukungu kama dithane m45 na ridomil mz.
· Kuweka shamba safi
· Kuteketeza mabaki ya vitunguu
· Kumwagiliaji maji nyakati za asubuhi au jioni


c) Kinyausi (Damping – off)
Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi na kuenezwa na udongo, mbegu na masalia ya mazao. Ugonjwa huu unasababisha mbegu kuoza kabla ya kuota na kunjauka kwa miche baada ya kuota. Ugonjwa unajitokeza hasa kitaluni ikiwa hali ya hewa ina unyevunyevu na udongo una maji maji.



Njia za kudhibiti ni kama zifuatazo:-
· Mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya thiram
· Kutumia mzunguko wa mazao
· Kusia mbegu kwa nafasi za kutosha
· Kuepukana na kubananisha miche kitaluni
· Kuepukanana na kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu


d) Virusi njano vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)

Ugonjwa huu unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu mafuta).
Dalili za ugonjwa ni:-
· Mistari ya rangi ya manjano kwenye majani.
· Kujikunja kwa majani
· Majani kugeuka rangi ya manjano na kuanguka
· Mimea mzima kudumaa, kujikunja na kufa.


Njia za kudhibiti ugonjwa huu ni:-
· Kutumia mbegu safi
· Kuweka shamba katika hali ya usafi
· Kuzuia wadudu kwa kupulizia dawa kama selecron, actellic, dursban nk.
Muhimu


Mara nyingi mimea ya vitunguu swaumu huwa havishambuliwi na wadudu mara kwa mara a mara ila kinga ni muhimu kuliko tiba


UVUNAJI Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja. SOKO Soko lipo kwasababu Vitunguu Swaumu ni kiungo kinacho tumika na wengi, kwa bei ya shiling 3,000 – 3800 kwa kilo
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.





No comments:

Post a Comment